Monday, September 28, 2015

NHC YAIBUKA TAASISI YENYE UWAZI ZAIDI MIONGONI MWA TAASISI ZA UMMA NA KUWA KINARA NA KUNYAKUA TUZO YA MISA-TAN YA UFUNGUO WA DHAHABU Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya Cheti cha Ufunguo wa Dhahabu, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya (kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa leo jijini Dar es Salaam.
Utafiti ulioipa NHC ushindi ulifanyika kwenye Wizara na Taasisi za Umma nane, kwa kipindi siku 21 kuanzia Juni 9 mpaka Juni 30, 2015, ambapo watafiti binafsi walifika katika taasisi hizo na kuwasilisha maombi yaliyotakiwa kujibiwa ndani ya siku 21, baadhi ya barua ziliandikwa kwa kiingereza, lakini kwa ufafanuzi zaidi nyingi ziliandikwa kwa kiswahili. 
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo alisema miongoni mwa masuala yaliyoifanya NHC kutwaa tuzo hiyo ni kutokana na 
uwazi katika mifumo yake ya ndani ya taarifa, kuwa tovuti inayotoa taarifa zote muhimu, matumizi makubwa ya mitandao ya jamii ya facebook, twitter, Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika mambo yanayolihusu Shirika, Kituo kwa huduma kwa wateja ambapo wateja hupata majibu ya papo kwa papo na au kuelekezwa kwa kitengo husika.
 Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Utafiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
Tuzo ya Cheti cha Ufunguo wa Dhahabu iliyokabidhiwa kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), miongoni mwa mambo makuu yaliyoipa NHC tuzo hiyo ni uwazi katika mifumo yake ya ndani ya taarifa, kuwa tovuti inayotoa taarifa zote muhimu, matumizi makubwa ya mitandao ya jamii ya facebook, twitter, Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika mambo yanayolihusu Shirika, Kituo kwa huduma kwa wateja ambapo wateja hupata majibu ya papo kwa papo na au kuelekezwa kwa kitengo husika.
  Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapisho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini, kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni mmoja wa wadhamini wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama  na kulia ni  Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti.
Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akionyesha ripoti iliyozinduliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa chapisho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini, kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni mmoja wa wadhamini wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama  na kulia ni  Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti.

 Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya cheti cha Kufuli la Dhahabu kwa 
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Wizara 
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
,  Anthony Ishengoma

kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2015 iliyokwenda kwa Wizara hiyo.
 kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa leo jijini Dar es Salaam 
 Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya (kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandhishi wa habari wakifuatilia shughuli nzima iliyokuwa inaendelea kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo jijini Dar es Salaam. 
Post a Comment