UTASHI WA KISIASA WAHITAJIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAENDELEO ENDELEVU (SDGS) YA 2016-2030

 Meneja wa Program wa Restless Development,Oscar Kimaro akizungumza na vijana (Hawapo Pichani )kutoka asasi mbalimbali kuelelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyofanyika katika Makao Makuu Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Asasi ya Hope Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015 Tanzania,Tumaniel Mangi  akizungumza na vijana  (hawapo pichani) juu ya kuwa mabalozi wa malengo 17 ya SDGs katika mkutano  uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakiwasha mishumaa kuashirishia kuonyesha njia ya utekelezaji wa Malengo 17 ya SDGs, katika mkutano  uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.     
     Picha na Emmanuel Massaka.


Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
LEO Septemba 25 hadi 27, wakuu wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana jijini New York, Marekani  kwa ajenda ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanayoanzia 2016 -2030.

Katika mkutano huo, nchi wanachama watapitisha ajenda za (SDGs) zenye Malengo 17 ya ambayo ni kukomesha umaskini, kuhamasisha usawa na kupinga uonevu, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,Afya Bora,Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Ujengaji wa Uchumi na Ajira zenye staha,Uboroshaji wa Majiji na Mitaa,Mahusiano ya Kimataifa ,Utawala wa Sheria na Haki na mengine mengi kufikia mwaka 2030.

Malengo hayo ni dira ya Ulimwengu na kufika mwisho kwa malengo Nane ya Millenia katika kupambana na umaskini ambayo ulimwengu uliazimia kutafikia kwa mwaka 2015.

Meneja wa Program wa Taasisi ya Restless Develoment,Oscar Kimaro amesema malengo ya  SDGs  ni vijana na wanawajibu kuwa mabalozi  kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa  kutokana na kuwepo kwa changamoto zinazoikabili kama nchi.

Kimaro akizungumza katika mkutano wa vijana katika kuelekea malengo ya SDGs amesema vijana wanakabiliwa na changamoto kubwa likiwemo suala upatikanaji wa elimu.

Katika Mkutano wa vijana waliwasha mishumaa kuonyesha njia kwa malengo hayo na viongozi  kuweza kuridhia kama nchi haiwezi kujitenga katika dira hizo ambayo dunia inaatamia.

Mkurugenzi wa Asasi ya Hope Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015 Tanzania,Tumaniel Mangi amesema  malengo ya SDGs yana ushirikishwaji hivyo inahitaji utashi wa kisiasa kusukuma malengo hayo.

Mangi amesema vijana ni sehemu ya kuleta msukumo chanya kwa kuyasemea masuala ya SDGs kuanzia ngazi ya chini  kutokana na ushirikishwaji uliopo wa malengo hayo.

Comments