Tuesday, September 29, 2015

CHOPA YA CCM YATUA MANYARA,MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUKUSANYA KURA ZA CCM

Mwigulu Nchemba mmoja ya wajumbe 32 wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akisalimiana na Wananchi wa Karatu Mjini jioni ya leo alipofika kwaajili ya Kuomba kura kwaajili ya Rais,Mbunge na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi.
Sehemu ya Wananchi wa Karatu Mjini waliofika Uwanjawa Mazingira Bora kusikiliza Mkutano wa hadhara wa Mwigulu Nchemba.
Mwigulu Nchemba akitoa darasa kwa Wananchi wa karatu kuhusu biashara ya Kumuacha Dr.slaa na kumpatia Edward Lowassa aliyehamia kutoka CCM. Dr.slaa aliyetumia Jasho na Damu kuuimarisha Upinzani wenye meno,Hii leo ameondolewa kwakuwa DILI imewekwa mezani ili Mtu mwenye kashafa mbalimbali chafu aweze kuwania Urais. Kwaaina ya Mgombea waliosimamisha UKAWA,Mwigulu amesema itakuwa rahisi sana kwa Magufuli kushinda kwa asilimia kubwa sana ya Kura.
Wananchi wa Mbulu Vijijini wakisikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba wakati akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Bashinet Mbulu Vijijini wakati alipokwenda kumuombea Kura Rais Mtarajiwa J.Pombe Magufuli na kuwanadi Madiwani na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Manyara.
Post a Comment