Tuesday, September 29, 2015

DKT FENELA MUKANGARA KUPAMBANA NA KERO YA MAJI KATIKA JIMBO LA KIBAMBA

 ………………………………………………………………………………..
Na Jimmy Kagaruki
 
Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM)
DKT FENELA MUKANGARA amesema atashirikiana na wananchi wa jimbo la kibamba
kupambana na kero ya maji kwenye jimbo hilo.
Akizungumza  na nuru fm MUKANGARA amesema
licha ya mikakati ya serikali ya kupambana na kero ya maji kwa wakazi wa jiji
la dar-es-salaam na jimbo la kibamba kwa ujumla bado kuna upungufu wa maji kwa
wakazi hao.
Ametaja sababu za upungufu huo wa maji kuwa ni pamoja na baadhi ya wananchi
wasio waaminifu kujiunganishia mitandao ya maji kiholela kwa ajili ya biashara
na uchakavu wa mabomba kutoka mtambo mkubwa wa maji wa ruvu juu.
MUKANGARA ameongeza kusema kuwa suala la wananchi wote kufikishiwa maji
majumbani litachukua muda na hivyo kusisitiza nguvu ya pamoja itumike kutoka
serikalini na wadau wa sekta ya maji na wafadhili kushirikiana kuchimba visima
virefu na vifupi ili kukabiliana na kero hiyo.
Aidha kutokana na umuhimu wa maji, MUKANGARA ametoa rai kwa wananchi wa jimbo
la kibamba kutoa taarifa kwenye mamlaka husika dhidi ya wale wote wanaohujumu
miundo mbinu ya maji ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

No comments: