Jengo la Biashara wa Lumumba Complex ambalo ni miongoni mwa majengo machache marefu mkoani Kigoma linavyoonekana kwa mbali mjini Kigoma jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole mjini Kigoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya (wapili kulia), Mbunge aliyemaliza muda wake wa Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba (wanne kjshoto), Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Aman Kabouru.
Rais Jakaya Kikwete,
Waziri wa Ardhi, Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu NHC, Mchechu na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Machibya wakifurahi mara
baada ya kukata utepe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa NHC Lumumba Complex mjini Kigoma Septemba 14, 2015. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, (watatu kushoto), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi, (wanne kushoto), Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya, (Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemia Mchechu (kulia), na kushoto ni Mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe katika jiwe kuashiria kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa National Housing Lumumba Business Complex mjini Kigoma. Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.
Umati wa wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment