Saturday, September 19, 2015

DK MAGUFULI ATINGA KIJIJINI KWAKE CHATO , AZURU KABURI LA ALIYEKUWA MWALIMU WAKE WA DARASA LA KWANZA BIHARAMULO


 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi  kwa wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera . PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wakazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakati wa mkutano wa kampeni
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba za Dk Magufuli wilayani Kakonko, Kigoma

 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea ubunge jimbo la Kakonko, Christopher Chizza wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Kakonko, Kigoma.
 Vijana wakisikiliza kwa makini wakati huku wakiwa juu ya baiskeli wakati Dk Magufuli akijinadi  wilayani Kakonko
 Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Cornel Pastory alipozuru kaburi la mwalimu huyo wilayani Biaharamulo
 Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastrory  alipkwenda kuzuru kaburi
 Mwalimu Cornel Pastory enzi za uhai wake
 Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory
 Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli wakati wa mkutano wa  kampeni mjini Biharamulo
 Mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kusini kupitia CCM, Profesa Anna Tibaijuka (kulia) akiwa miongoni mwa walioshiriki katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Biharamulo
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akifanya kampeni mjini Biharamulo
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini ili wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Biharamulo
 Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa  Bi9aharamulo baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa kampeni mjini humo.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Biharamulo, Oscar Mkassawakati wa kampeni hizo.

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Chato,Meedard Karemani katika Kata ya Igalula  wilayani Chato ambaye ndiye mrithi wake katika nafasi hiyo

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nyumbani kwa Dk Magufuli, mjini Chato

 Sura zikionesha matarajio makubwa  baada ya kumuona Dk Magufuli alipowasili katika Kata ya Igalula alipozungumza nao na kupata wasaa kuwaaga wananchi wa Jimbo la Chato baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kugombea urais wa T anzania.

 Sehemu ya wananchi wa Chato wakimlaki Dk Magufuli
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa baada ya Dk Magufuli kuwasili nyumbani kwake Chato baada ya kufanya kampeni katika Wilaya ya Biaharamulo, Kagera.
 Dk Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa
 Dk Magufuli akisalimiana na ndugu zake akiwemo mamake mzazi (katikati) alipowasili nyumbani kwao Chato baada ya safari ndefu ya kufanya kampeni katika mikoa 13 nchini.
Dk Magufuli akisalimiana na ndugu nyumbani kwake Chato

Post a Comment