PPF YAVUNA WANACHAMA WAPYA KWENYE WIKI YA WAFANYAKAZI WA AIRTEL, (AIRTEL HR WEEK)

 Mfanyaakzi wa Airtel, (kulia), akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ufunguzi wa wiki ya Wafanyakazi wa Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.

 Wafanyakazi wa Airtel, wakipatiwa maelezo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na PPF, wkati wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya simu makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.
 Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, (kulia), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, wakatyi wa ufunguzi wa wiki ya Wafanyakazi wa Airtel

NA K-VIS MEDIA
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umevuna wanachama wapya kadhaa kwenye Wiki ya Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, iliyoanza leo Septemba 26, 2015 pale makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam.
Akizungnumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi hao, Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, amesema, Airtel ni moja ya “Akaunti’ kubwa za PPF, kwa maana ya Mfuko kuwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka kampuni hiyo, hivyo wameitumia fursa hiyo kutoa elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
“Pamoja na kusajili wanachama wapya chini ya Mpangop wa Wote Scheme, yaani ucnangiaji wa hiari, pia tumewaeleza wanachama wetu kuhusu mafao mapya yatolewayo na Mfuko kama fao la Uzazi.” Alifafanyua Ngowi.
Meneja Msoko huo wa PPF pia alisema, Wanachama wa PPF kupitia mpango huo wa wote scheme, wanaweza kujiunga na bima ya afya ya NHIF, ambapo PPF inakuwa mdhamini wa wanachama wake kupitia mpango huo wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme).
 Afisa Uwekezaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo, (kulia), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, wakati wa utoaji huduma kwenye wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
 Afisa wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Saluna Aziz Ally, (kushoto), akimeuelekeza Mwanachama wa Mfuko huo jinsi ya kupata taarifa za michango yake kupitia simu ya mkunoni, huduma ijulikanayo kama “PPF Taarifa), wakati wa ufunghuzi wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel, iliyoanza leo Sptemba 26, 2015 pale makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, Morocco jijini Dar es Salaam
 Mwanachama mpya wa PPF Sitti Mweneyuni, akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam
 Mwanachama mpya wa PPF akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam

Comments