Tuesday, September 15, 2015

ABDULRAHMAN KINANA: DR JOHN POMBE MAGUFULI NI SULUHISHO LA MATATIZO YA WATANZANIA

1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora tayari kwa kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jana, huku makada mbalimbali wa cCM wakichagiza kumpigia debe Dr. John Pombe Magufuli
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewambia  wananchi wa Tabora  hakuna haja ya kuhangaika na upinzani kwani jibu la utatuzi wa matatizo ya watanzania ni Dr. John Pombe Magufuli hivyo wanatakiwa kumpigia kura za ndiyo Dr. John Pombe Magufuli ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wakati utakapofanyika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini kote(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-TABORA)
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Samwel Sitta mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni CCM.
3
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Tabora jana katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
4
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi wa mjini Tabora kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
5
Umati wa wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia mjini Tabora jana.
6
Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Samweli Sitta ambaye ni mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni CCM wakati wa mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
7
Msanii Mr Blue akitumbuiza katika mkutano huo.
8
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya kampeni ya CCM Mzee Samwel Sitta akiwahutubia wananchi wa mjini Tabora katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana.
9
Mjumbe wa kamati ya Ushindi ya Kampeni CCM Ndugu Steven Masele akiwahutubia wananchi wa mjini Tabora jana.
10
Kada wa CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Bw. Amon Mpanju akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
11
Kundi la TOT likifanya vitu vyake jukwaani.
12
Msanii Ali Tumbo na wasanii wenzake wakikamua jukwaani katika mkutano huo.
13
Ndugu Emmanuel Mwakasaka mgombea ubunge akizungumza kwa niaba ya  wenzake katika mkutano huo na kuomba kura za ndiyo kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo.
14
Msanii wa Komedi Orijino Masanja Mkandamizaji naye akafanya mambo yake akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli.
15
Kutoka kulia ni Joti, Wakuvanga na Shemejiii wasanii wa kundi la Orijino Komedi wakifanya vitu vyao jukwaani.
16
Msanii Rich Mavoko akipagawisha wananchi katika mkutano huo.
17
Emmanuel Mbasha naye akaonyesha uwezo wake jukwaani.
18
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli na Mgombea ubunge wa jimbo la Tabora mjini  Ndugu Emmanuel Mwakasaka wakionyesha ilani ya uchaguzi ya CCM katika mkutano huo baada ya mgombea huyo kukabidhiwa ilani hiyo
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akitoka kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kuhutubia mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Post a Comment