Friday, September 18, 2015

NCHI ZA AFRIKA ZIMEASWA KUIMARISHA MAWASILIANO KATIKA UTOAJI WA TAARIFA ZINAZOHUSIANA NA MAGONJWA YA MAFUA MAKALI

x1
Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate akuitoa hotuba ya ufungua wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
x2Baadhi ya washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
x3Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate (aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Semina hiyo.
…………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali yanayosababishwa na virusi vya influenza ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya Dkt. Custodia Mandlhate alipokuwa akifungua semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, semina hiyo inayoendelea jijini Nairobi.
Mawasiliano ya haraka wakati wa dharura za kiafya yanahusu ngazi zote kuanzia kimataifa wakati wa hatari ni yetu sote, ni ya kimataifa, kikanda na kitaifa, hivyo basi kipaumbele cha WHO ni kuhamasisha watu, mashirika na serikali kushiriki katika kutoa taarifa na elimu juu ya namna ya kuokoa maisha ili kuchukua hatua sahihi za kuzuia,  kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa huo” alisema Dkt. Custodia.
Dkt. Custodia alisema kuwa hatua ya kupata elimu sahihi ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo inatekelezwa kwa kupitia matumizi bora ya mawasiliano ya umma juu ya afya, ushiriki wa jamii na uhamasishaji wa kijamii kwa kutumia vyombo vya habari, sera na tafiti zinazofaywa ili kuokoa maisha ya watu katika eneo husika.
Malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uwezo washiriki ambao utaimarisha mawasiliano kwa watoa maamuzi muhimu ya kitaifa na kikanda katika kuimarisha hatua za dharura katika kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa wa mafua makali.
Malengo mengine ni pamoja na washiriki kupata uelewa juu ya njia bora za kutoa taarifa wakati inapotokea hatari ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya ambayo yanahitaji dharura katika utekelezaji wake pamoja na kuimarisha mitandao ya kikanda ya watoa maamuzi na watendaji ili kubadilishana uzoefu na utaalamu kupitia nchi wanazoziwakilisha.
Kwa upande wake muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania Dkt. Vida Makundi alisema kuwa semina hiyo ina manufaa makubwa kwa taifa hilo kwa kuwa nchi hiyo tayari ina viashiria vya kuapata yanayotokana na wanyama yakiwemo mafua makali ya ndege na mengine hivyo hivyo ni vema kujifunza na kuchukua tahadhari ikiwaa ni pamoja na kuelimisha jamii namna ya kujikinga majanga mbalimbali ya magonjwa na matukio yanayoathiri afya ya binadamu yanapotokea.
Dkt. Vida alisisitiza kuwa wataalamu wa afya na sekta nyingine zinzohusika na afya ya binadamu wakaelewa kuwa ili kufanikisha mawasiliano kwa jamii hawana budi kushirikiana kwa karibu na  wanahabari kutoa habari kwa jamii ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa ambapo kunahitajika kuwepo na uelewa mpana wa kisiasa, kijamii na kiutamaduni na kuzingatia eneo lililoathiriwa na ugojwa wa mlipuko.
Mkutano huo unaoendelea Nairobi nchini Kenya unaongozwa na kaulimbiu inayosema “Okoa maisha na zuia ugonjwa kuenea” unajumisha ya zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi 21 zilizopo katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo washiriki wanatoka katika Wizara za Afya, Habari na Muwakilishi mmoja wa WHO kutoka nchi anayowakilisha katika ukanda huo.
Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Msumbiji, Malawi, Botswana, Lesotho, Sudani ya Kusini, Madagaska, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Swaziland, Rwanda, Mauritius, Eritrea, Namibia, Ethiopia, Afrika Kusini na Zimbabwe.na Kenya ambayo ni mwenyeji wa semina hiyo.

No comments: