Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (kulia) akizungumza jana Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya onesho la Swahili International Expo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet Jimmy Kibati kama mmoja wa wadhamini.
Mratibu wa onesho la Swahili International Expo Philip Chitaunga (kulia) akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu onesho hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Wenginekutoka kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet kama mmoja wa wadhamini, Kaimu Mkurugenzi TTB Devotha Mdachi na Milat Mekennon kutoka shirika la ndege la Ethiopia.
ONESHO la Swahili International Expo linatarajiwa kufanyika wiki hii, kuanzia tarehe 1-3 Oktoba,2015 katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Hii ni mara ya pili kwa Onesho hili kufanyika,Mwaka jana ilikuwa mara ya kwanza October 1- -4,2014
Onesho la mwaka jana liliweza kuwavutia Waoneshaji 40,Mawakala wa Utalii walioalikwa kutoka nje ya nchi 19 (hosted Buyers),Waaandishi wa Habari kutoka nje ya nchi 4 (media),Wageni waliotembelea onesho hilo 1,200,Wadhamini 40 na Mdhamini mkuu alikuwa Ethiopian Airlines
Mwaka huu Waoneshaji ni 100,Mawakala wa utalii na waandishi wa habari walioalikwa 43, Wageni wanaotegemewa kutembelea onesho 2,000,Wadhamini 41 na Wadhamini wakuu wamegawanyika katika makundi.
Kuna Platinum Category ambao ni Ethiopian Airlines – Mdhamini Mkuu (usafiri kwa ajili ya mawakala wa nje walioalikwa)
Pia kuna Gold Categoryambao ni Fast Jet Airline Limited, An’gata camps Ltd, FB cars Ltd, Gibbs Farm,Ramada Resort Dar es ssalaam, SAA North America, Seacliff Hotel, Sopa Lodges and Spicenet Tanzania .
Kwa upande mwingine kuna Silver category ambao ni Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Antelope Tours and Safaris, Azam Marine, Congema Tours and safaris Ltd, Fernandes Tours & safaris, Melau Tours & Safaris Ltd, Precision Air Services, Shirika la ndege la Qatar, Rwandair, Shirika la ndege la Afrika Kusini , Shidolya Tours & Safaris Ltd, Sun Tours &travel Lts and Shirika la ndege la Uturuki.
Wengine ni BougainvillaSafari Lodge, Ledgar Plaza Hotel, Cenizaro Hotels & Resorts, Emerald Collection Zanzibar, Essque zalu Zanzibar, Holiday Inn Dar es salaam, Kudu Lodge, Kunduchi bBeach Hotel, Manyara Wildlife safari Camp, Maru Maru Hotel, Mberesero Lodges & Tented Camps, Melia Zanzibar, Neptunes Hotels, New Africa Hotel, Ocean Paradise Resort & Spa, PlanHotel Hospitality Group, Protea Hotel Courtyard, Seacliff Court Hotel & Luxury Apartments, Seacliff Resort & Spa Zanzibar, Serena Hotel, Southern Sun Dar es salaam, White Sands Hotel.
Black tomato, Boogle Woogle, Cultural Art Center,Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.
Kwa upande mwingine kutakuwa na kitengo cha Hosted Buyers Programme ambapo Programme Maalum ya kuwatembeza mawakala wa Utalii katika maeneo Wageni hao watatembelea Zanzibar , Lake Manyara na Ngorogoro.Lengo ni kuona, kujifunza kuhusu utalii wa Tanzania, na kuonja (kuexperience ) ukarimu wetu.
Pia kutakuwa na kitengo cha Cultural Village ambalo ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya maonesho ambapo wajasirimali wadogo wataweza kuonesha bidhaa na huduma zao.
Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Tinga Tinga, Wachongaji vinyago, watengenezaji wa Sanaa mbalimbali, wanamitindo, vikundi vya burudani muziki wa bendi na burudani (Utalii Band) na Kikundi cha utamaduni kutoka Chuo cha Tumaini , Arusha .Pia kutakuwa na Nyama Choma (wageni wataweza kupata vyakula vya kitanzania )
Kwa ujumla TTB inawataka watanzania watembelee onesho hilo kutokana na ukweli kwamba onesho la S!TE ni fursa ya kuhamasisha utalii wa ndani,Watoa huduma mbalimbali za kitalii watakuwepo, wataweza kutumia fursa hiyo kutoa maelezo kuhusu huduma zao na kuwahamasisha watanzania kutembelea maeneo ya kitalii (vikundi mbalimbali vitawea kuhamasika –wanafunzi, wafanyakazi nk)
Comments