Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Tuntufye Mwambusi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mauzo ya nyumba za makazi za Shangani mjini Mtwara .
Nyumba za makazi za Shangani Mtwara kama zinavyoonekana sasa.
Nyumba za makazi za Shangani Mtwara kama zinavyoonekana zitakapokamilikaNyumba za makazi za Shangani Mtwara kama zinavyoonekana zitakapokamilika
Nyumba za makazi za Shangani Mtwara kama zinavyoonekana zitakapokamilika
Nyumba za makazi za Shangani Mtwara kama zinavyoonekana zitakapokamilika
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI UUZWAJI WA NYUMBA ZA SHANGANI, MTWARA
Kwa
mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Jumatano, 16,
Septemba, 2015) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa
Shangani, Mtwara. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2013 na
unatarajiwa kukamilika rasmi mwisho wa mwezi ujao, ikiwa ni miezi 24 baada ya
kuanza ujenzi. Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Sh 4.8 bilioni
mpaka utakapomalizika.
Mradi
huu upo katika eneo tulivu la Shangani Mkoani Mtwara takribani kilomita moja kutoka katikati
ya mji na upo karibu kabisa na bahari ya Hindi. Mradi huu una nyumba 30 za
kuuzwa zilizopo kwenye majengo matatu ya ghorofa 5 ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii. Usalama pia
umezingatiwa kwa wakazi na wanunuzi wa Mradi huu kwa kuweka uzio mkubwa
Nyumba
10 kati ya hizi 30 zimeshafanyiwa
booking na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). kila nyumba ina vyumba vitatu vya kulala,
kimoja kati ya hivyo ni cha kulala kinachojitegemea, sebule iliyoungana na eneo
la kula chakula, choo cha umma na jiko kubwa la kisasa. Nyumba hizo zina ukubwa
wa aina mbili yaani zile za ukubwa wa mita za mraba 117.2 (sq.m) na zingine za
ukubwa wa mita za mraba 182.6
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka na eneo kubwa
la ziada la maegesho ya magari pamoja na Club House.
Kila
nyumba itauzwa kwa bei ya TZS
190,127,000 bila VAT na TZS
224,349,860 ikiwa na VAT. Tunawahamasisha na kuwakaribisha Watanzania wote
walio nchini na wanaoishi nje ya nchi wafanye mawasiliano na ofisi zetu za
Makao Makuu ya Shirika, ofisi zetu za mikoa, au kupitia barua pepe na
kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato.
Uzinduzi
wa mauzo ya nyumba za mradi huu ni mfululizo wa uzinduzi wa miradi ya NHC
unaolenga kutimiza malengo ya mkakati wa Shirika wa miaka kumi 2015/16 –
2020/25.
Ukiwa
mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayehitaji kununua nyumba
katika mradi huu, tafadhali waweza tumia akaunti nambari 1001962018 iliyopo
Bank ABC au wasiliana na kitengo cha mauzo simu namba 0754 444 333; barua pepe:
sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA
HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
No comments:
Post a Comment