MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI LINDI


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, Septemba 23, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo lake hilo, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, Septemba 23, 2015.
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakimshangilia Mgombea Ubunge wao, Salum Barwany, alipokuwa akihutubia na kukonga nyoyo zao kwa kugusa moja kwa moja changamoto zinazowakabili na namna watakavyoweza kuzitatua iwapo watapata ridhaa ya uongozi.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akifurahi jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany.
Uwanja wa Pilipili ulikuwa ni shangwe tupu, muda wote wa Mkutano.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, Septemba 23, 2015.
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, Septemba 23, 2015.

Comments