Monday, September 14, 2015

MFUKO WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA NANE YA MAFANIKIO Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Msokwa akiongea na waandishi wa habari  mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam juu ya maadhimisho ya miaka nane ya mafanikio ya TMF. Pembeni ni Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura na Afisa Mafunzo wa TMF, Radhia Mwawanga. 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza tukio hilo, alisema Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la madhimisho ambayo yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa habari waliowezeshwa na misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani zimechangia kuleta uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha kiwango cha mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala bora na haki za binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi waliowezeshwa na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Waandishi wa habari wakichukua tukio. --- Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) utaadhimisha miaka nane ya mafanikio katika kuongeza uwajibikaji kwa kuimarisha sekta ya habari nchini Tanzania kupitia tukio ambalo litafanyika jijini Dar es salaam.

 Tukio hilo litawaleta pamoja waandishi wa habari na wanataaluma wengine ambao wamewezeshwa na misaada ya TMF, wafadhili, wadau wa sekta ya habari pamoja na taasisi za kiraia na serikali. Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza tukio hilo, Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura alisema: “Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la madhimisho ambayo yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa habari waliowezeshwa na misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani zimechangia kuleta uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha kiwango cha mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala bora na haki za binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi waliowezeshwa na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya. 


Post a Comment