Wednesday, September 16, 2015

AMOS MAKALLA AAGA RASMI WIZARA YA MAJI

1

Mhe. Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Maji waliompokea mara baada ya kuwasili Wizarani, pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Gideon Manambo.
4
Mhe. Amos Makalla akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji, wakati akiaga wizarani hapo.
2
Mhe. Amos Makalla akiwa ofisini kwake, alipofika kuaga Wizara ya Maji.
3 
Mhe. Amos Makalla akipokea shada la maua kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Beatrice Patrick.
5
Mhe. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji.
………………………………………
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo mchana ameaga rasmi watumishi wa Wizara ya Majina kwenda kuanza majukumu mapya kama Mkuu wa Mkoawa Kilimanjaro.
Mhe.Makalla ambaye alifika Wizarani hapo, akitokea Ikulu alikoapishwa rasmi na Mhe. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe.Makalla ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji kwa zaidi ya mwaka mmoja, aliweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa licha kuwa mgeni kwenye Sekta hiyo. Ambapo aliweza kuzunguka karibu mikoa yote na kutembelea karibu Mamlaka zote za Maji nchini katika kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji.

No comments: