Tuesday, September 29, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA MTERA KWA KIBAJAJI, AWAAMBIA WANAMVUMI MSIDANGANYIKE

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Mvumi jimbo la Mtera wilaya ya Chamwino leo wakati akiendelea na kampeni zake katika majimbo ya Isimani mkoani Iringa, Kibakwe na Mtera  mkoani Dodoma, ambapo amewaomba wananchi hao kutohadaika na wagombea wanaowadanganya kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya kitu kwa miaka 54
Dk. Magufuli amesema kuwaambia watanzania CCM haijafanya kitu kwa  miaka 54 ni jambo ambalo linachekesha  kwani  Utulivu na amani  tuliyonayo  ni matunda ya uongozi bora wa viongozi wa serikali ya CCM waliopita wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, “Wanapita kwenye barabara za lami zilizojengwa na serikali ya CCM tena nikizisimamia mimi John Pombe Magufuli, Wanatumia miundombinu ya mawasiliano na Umeme uliosambazwa kwa zaidi ya  asilimia 40 nchini na serikali ya CCM lakini wanasema haijafanya kitu ni jambo la kushangaza.
Mbaya zaidi wamekuwa viongozi wa serikali  tena wakiwa na nyazifa kubwa serikalini,  sasa kama walishindwa kuwajibika  na kuwatumikia watanzania wakiwa serikalini kwa nini hawakuondoka  mapema, Lakini  muda wote wakabaki CCM wakisifia mafanikio hayo ambayo leo wanayaponda. Si sawa kabisa hao wanatafuta madaraka kwa kutaka kuwadanganya watanzania nawaasa msikubali kudanganywa waongo hawa.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-MVUMI-DODOMA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Isimani mkoani Iringa Mh. Willliam Lukuvi katika mkutano uliofanyika kata ya Pawaga.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Mvumi mkoani Dodoma leo.
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi akiwaomba kura wananchi wa kata ya Pawaga jimbo la Isimani katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais  Dk John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Nani kakwambia vijana hawapendi kwenda kwenye mkikutano ya CCM knaja huyu wa Migori alihudhuria katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM Irene Uwoya wa  kushoto akiwa katika mkutano wa kampeni wa Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika kata ya Migori jimbo la Isimani pamoja na wasanii wenzake kutoka  kulia ni Stara Thomas  na Jacob Steven
????????????????????????????????????
Wasanii hawa wakiwa tayari kwa kutoa burudani kwenye moja ya mikutano ya Kampeni ya Dk. John Pombe Magufuli katika jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mvumi kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano uliofanyika tarafa ya Mvumi mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakati mkutano huo ukiendelea.
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Mtera kupitia CCM Ndugu Livinstone Lusinde Kibajaji akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mamia ya wananchi waliohudhurua katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mzee John Samwel Malecela akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mji wa Mvumi mkoani Dodoma. 
????????????????????????????????????
Hapa ni Dk John Pombe Magufuli tu.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya kuikubali hotuba ya Dk John Pombe Magufuli alipohutubia mji wa Mvumi leo.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo.

Post a Comment