Wednesday, September 23, 2015

AIRTEL YAZINDUA KIFURUSHI CHA “YATOSHA NYTS” BILA KIKOMO

 Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na
Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya
ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja  kupiga simu
Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja
na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi
300 tu.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja  kupiga simu Airtel
kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na
kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300
tu. Kushoto ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

.     Wateja kupiga  simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo

·    Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi
·         Kwa shilingi 300 tu.
KAMPUNI ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha  MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.
Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima
kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda
mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi
siku za wikiendi.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde
alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti  ya huduma za
simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji
ya wateja wetu.
 Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa  kwa kuzingatia
mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku
inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao. “Yatosha
Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na
wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.
Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za
mawasiliano  bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa
kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia
kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi. Kwa shilingi
300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel
kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao
yote  na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku.
Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya
na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja
wake chini ya huduma ya kibunifu ya  Airtel Yatosha. Airtel Yatosha
inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia
huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.
Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel


Post a Comment