Tuesday, July 05, 2016

RAIS SHEIN ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA


S1Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiliamali  wanawake wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mke wa Rais wa awamu ya tatu Mama Anna Mkapa.
S2Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein  akipata maelezo toka kwa mjasiliamali juu ya vyakula vilivyosindikwa wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S3Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiangalia mafuta ya kula yanayotengenezwa na wajasiliamali , wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S4Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza swali kwa mjasiliamali wakati alipotembelea banda la wanawake Wajasiliamali  (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S5Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusiana na uzazi wa mpango, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S6Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S7Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S8Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Waziri  wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Balozi  Amina Salum Ali,wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.                 
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

No comments: