Thursday, July 14, 2016

SHINDANO LA DANCE%KURINDIMA MWEZI HUU CHINI YA VODACOM TANZANIA

 Mratibu wa Shindano la Dance 100% 2016, Brendansia Kileo(kushoto)na Jaji wa shindano hilo,Khalila Kells(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo(hawapo pichani)wakati wa kutangaza Uzinduzi na Udhamini wa shindano hilo litakaloanza tarehe 16 mwezi huu, Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania pamoja na Coco-Cola.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiteta jambo na majaji wa shindano la Dance 100% 2016,Super Nyamwela(katikati)na Khalila Kells,Wakati wa kutangaza Uzinduzi na Udhamini wa shindano hilo leo jijini Dar es Salaam,  litakaloanza tarehe 16 mwezi huu, Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania pamoja na Coco-Cola.

Shindano la Dance% kuanza kurindima mwezi huu
Vodacom yaendeleza udhamini wake kwa mwaka wanne mfululizo
Shindano kufanyika kwa miezi mitatu na Bingwa kuondoka na kitita kizito.

Mashindano ya  kucheza muziki ya vijana maarufu  kama Dance 100% yanayoandaliwa  na kituo cha televisheni cha East  Africa(EATV) yanatarajiwa kuanza Julai 16 mwaka katika viwanja mbalimbali jijini Da r es Salaam. Yakitangazwa wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam ambapo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza kuendelea kudhamini mashindano hayo.

Akiongea na waandishi wa habari,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikidhamini mashindano hayo kwa kipindi cha miaka minne mfululizo na katika msimu wa mwaka huu imejidhatiti kwa kuweza kuendeleza gurudumu la tasnia hii. 
Nkurlu alisema kuwa Vodacom imeendelea kudhamni shindano kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Aliongeza kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo, burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Alisema Nkurlu.

Aliwataka vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.

Naye Mratibu wa Shindano hilo kutoka kituo cha televisheni cha Afrika Mashariki ‘Brendansia Kileo alisema kuwa mashindano haya kwa msimu wa mwaka huu yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania na kampuni ya Coca-Cola kama kinywaji rasmi cha Dance 100% 2016. Mashindano haya yataanza kufanyika  jijini Dar es Salaam katika viwanja vya leaders club, mashindano yataanza na raundi tatu za usaili tarehe 16,23 na 30 Julai (2016) na kufuatia hatua za robo na nusu fainali na kasha Fainali. Aliyataka makundi ya dansi kujitokeza kujiandikisha kushiriki,Pia alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kushuhudia michuano ya usaili “LIVE’ bila kiingilio chochote.

“Huu ni mwaka wa Tano (5) East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya  na mara ya nne (4) chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki na washindi wakiwa vinara wakutangaza Dansi katika nchi mbali mbali kama T- Africa, The Chocolate, Wakali sisi na WD”Alisema Kileo .

Alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa yanafanyika wikiendi kwa muda wa miezi mitatu vilevile yatakuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila Jumapili saa  moja kamili usiku na kundi litakaloibuka na ushindi litajinyakulia kitita cha shilingi  Milioni saba (7) na mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi milioni (2) na mshindi wa tatu atapongezwa na shilingi milioni mmoja (1) tofauti na miaka ya nyuma.

No comments: