Saturday, July 23, 2016

DK. JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA CCM, AMCHAGUA TENA KINANA KUWA KATIBU MKUU

1Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM baada ya wajumbe hao Kumthibitisha kuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano Kwa kumpigia kura zote za ndiyo wajumbe waliopiga kura ni 2395 kura zilizoharibika ni 0 na Mwenyekiti Dk. John Pombe Magufuli ameshinda kwa kwa kupigiwa kura zote 2395, Lakini pia mwenyekiti  huyo ameamua kuendelea na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Sekretarieti nzima iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
2Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.
3Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita na  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
6Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza machache kutoka kwa  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo.
7Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipokea ilani ya uchaguzi kutoka kwa  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
89
Viongozi wastaafu wakiwa katika mkutano huo kutoka kushoto ni Mzee John Samwel Malecela, Mzee Amani Abeid Karum, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mohamed Gharib Bilal na Mzee Pius Msekwa.
10Viongozi hao wakiwa katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
11
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Ndugu Agustino Mrema akiwasliana na wake wa viongozi wastaafu.
12Baadhi ya wajumbe wakishangilia mara baada ya mkutano huo kumthibitisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM.
131415Mwanachama wa CHADEMA Mgana Msindai akiwapungia mkono wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM baada ya kurejea CCM alipotangaza rasmi kwenye mkutano mkuu huo.
16Mgana Msindai akielekea jukwaani ili kutangaza nia yake ya kurejea CCM leo kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma.
17Mzee John Momose Cheyo Mwenyekiti wa UDP aktoa salam zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.
18Freddy Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wa chama cha CHADEMA akitangaza nia yake ya kurejea CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma leo.leo.
19Mzee Yusuf Makamba akisalimiana na Mwanaye Januari Makamba Mzee Makamba alikuwa ni kivutio kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutokana na hotuba yake aliyoituma leo.
20Mzee Yusuf Makamba akisalimiana na baadhi ya wake wajumbe wa mkutano huo.
21Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akijadi;iana jambo na  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma leo .

No comments: