Friday, July 01, 2016

KLABU YA SIMBA YAWATAMBULISHA KOCHA MPYA NA KATIBU MKUU MPYA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR

Rais wa klabu ya Simba,Evans Aveva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuwatambulisha katibu mkuu mpya wa klabu ya Simba bwana Patrick Kahemele (mwisho kushoto) na kocha mkuu mpya Joseph Omog (pichani kati) ambae ni raia wa Cameroon.Kocha Omog aliwasili jana usiku hapa jijini..
Pichani wa tatu kulia ni Katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele akifafanua jambi na kwamba kuanzia sasa ndiye atakaehusika na masuala ya klabu hiyo,kwani kwa kipindi kirefu timu hiyo haikuwa na Mtendaji Mkuu ambaye amekuwa akishugulikia masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa ujumla. 
Kocha Mkuu mpya Joseph Omog,ambae ni raia wa Cameroon akifafanua jambo mbele ya wana habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini  humo .Picha na Michuzi Jr.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

KLABU ya Simba imemtambulisha kocha mpya leo na kuingia nae kandarasi ya miaka miwili 2016/2018 huku wakimpa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi. Raisi wa Simba Evance Aveva amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kupitia sifa za Joseph Omog na kuona atakuwa msaada mkubwa sana katika kuisaidia timi ya Simba.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa kocha huyo, Aveva amesema huu ni mwanzo mzuri kwa Simba wana imani ana nafasi kubwa ya kuwasaidia katika namna watakavyobadilisha na kupata mafanikio kwa timu hiyo. " Ni mategemeo yetu kuwa kandarasi hii tuliyoingia na Omog itakuwa na mafanikio na malengo makubwa ya Simba ni kuitoa ilipo na kuirudisha kuwa ya zamani, ". Naye Omog amesema kuwa amekuja Simba kwa ajili ya kuisaidia na kuijenga na atafanya kazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa.

Wakati huo huo Aveva alimtambulisha katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele ambaye kuanzia sasa atahusika na masuala ya klabu hiyo na zaidi kwa kipindi kirefu hakukuwa na mtendaji mkuu ambaye anakuwa anashughulikia suala la utendaji kiujumla. 

Kahemele amesema kuwa, Simba kuna changamoto kubwa sana na malengo yake ni kuitoa ilipo na kuirudisha ilipokiwa zamani na amewahakikishia wanachama wa Simba wote kuwa atashirkiana vizuri na kamati ya utendaji katika kulitekeleza hilo na ndiyo maana hata viongz walimfuata ili waweze kusaidiana. "Nawaahidi kufanya kaz usiku na mchana na katika.msimu unaoanza nitahakikisha tunakwenda kwa kasi na zaidi wameleta kocha mzuri anayejua majukumu yake na mimi nitajibika kulingana na nafasi yangu,".

Kahemele amesema Simba wana mtaji mzuri wa wanachama na watatumia nafasi hiyo kuwa faida kwao kwani wanaweza kufanya mambo mengi kwa fedha za wanachama hao hao.
Post a Comment