Saturday, July 16, 2016

MASANJA KUNGU KADOGOSA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA TRL


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amemteua  Bw. Masanja Kungu Kadogosa(pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya Reli Tanzania(TRL). Uteuzi huo umeanza Julai 01, 2016.
Bw. Kadogosa, mwenye umri wa miaka 41,  mapema Februari 4, 2016 aliteuliwa na Serikali kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL baada ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa awali Mhandisi Elias Mshana kuanza likizo ya kustaafu.
Aidha kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa juu katika TRL Bw. Kadogosa alikuwa Mkurugenzi wa Mikopo katika Benki ya ya Maendeleo ya TIB.
 Kitaaluma Mkurugenzi huyo mpya ni msomi wa Masuala ya Uhasibu, Usimamizi wa Fedha  na Benki akiwa na Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara aliofuzu katika Chuo kikuu cha Umea mwaka 2004 nchini  Sweden. 
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Ofisi ya  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Dar es Salaam,

Julai 15, 2016

No comments:

KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KITUO CHA MALIKALE – MTWA MKWAWA, IHINGA, IRINGA

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji ,  amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Malikale ch...