Saturday, July 23, 2016

MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM UNAENDELEA MJINI DODOMA

jk
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. Jakaya Kikwete akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu Maalum kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma, ambapo mkutano huo utamthibitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli aliyekaa kulia kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa akipokea uongozi huo kutoka kwa mtangulizi wake Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi  Dk. Jakaya Kikwete, Wajumbe wengi wamehudhuria katika mkutano huo wanatarajia kupiga kura hiyo muda wowote kuanzia sasa
Kushoto  ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara , Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wa pili kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA
9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa maelezombalimbali  na kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama Dk Jakaya Kikwete  katika Mkutano Mkuu Maalum  ili kuufungua tayari kwa  kumthibitisha
001Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM Dk. John Pombe magufuli wa pili kutoka kushoto akishiriki kuimba wimbo wa taifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM anayeng’atuka madarakani Dk. Jakaya Kikwete wa pili kulia wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar wa tatu kutoka kushoto, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM taifa Mzee Benjamin William Mkapa na kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
1Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Ali Hassan Mwinyi akishiriki kuimba nyimbo kabla  wakati wa mkutano huo.
2Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar SMZ Mhe. Mohammed Said Mohammed Dimwa
3Mama Salma Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka mkoa wa Lindi akishiriki kuimba nyimbo za hamasa na pamoja nawake wa viongozi wenzake.
4Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Part TLP Bw. Agustino Lyatonga mrema na viongozi wenzake wa vyama vilivyoalikwa katika mkutano mkuu Maalum wa CCM unaofanyika  mjini Dodoma
5Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar SMZ Mhe. Mohammed Said Mohammed Dimwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki kuimba nyimbo za hamasa.
6Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiwa katika mkutano huo.
7Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kushoto na Mzee Said El Maamry na wageni waalikwa wengine wakiwa katika mkutano huo.
8Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akiwa na wajumbe wenzake kutoka mkoani Mwanza wakiwa katika mkutano huo, Kulia ni Richard Ndasa na wa tatu ni Ndugu John Mongela.
16Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Iringa kutoka kulia ni Dk Agustine Mahiga na  Salim Abri Asas pamoja na wenzao wakiwa katika mkutano huo.1Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma
2Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma sasa hivi.
3
Baadhi ya wake wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo
4
Baadhi ya viongozi wastaafu wakipitia gazeti la uhuru lenye makala maalumu ya Dk. John Pombe Magufuli anayetarajiwa kuthibitishwa leo kuwa Mwenyekiti wa Cma cha Mapinduzi CCM.
5
Wajumbe kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
7
Wajumbe kutoka mkoa wa Morogoro nao hawakuwa nyuma kupitia makala ya Gazeti la Uhuru leo.
8
Mwimbaji wa kundi la Hamasa la CCM TOT Bi. Khadija Kopa na waimbaji wenzake wakitumbuiza katika mkutano huo.
9
Mmoja wa waalikwa akipata kumbukumbu katika mkutano huo.
10
Kundi la Hamasa la TOT likiendelea na burudani katika mkutano huo.
1112
Baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Mjumbe Angela Kairuki kutoka mkoa wa Dar es salaam wakiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
13
Dk. Fenella Mukangara kutoka mkoa wa Dar es salaam na Tambwe Munde kutoka mkoa wa tabora  wakiserebeka pamoja na wajumbe wenzao.
14
Mjumbe Munde Tambwe akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba.
15
Mjumbe Fredrick Mwakalebela kutoka mkoa wa Iringa akiwa na wajumbe wenzake.
17
18
TOT ikiendelea kutumbuiza
1920
Mwakipesile na Mary Mwanjelwa Wajumbe kutoka mkoani Mbeya wakisalimiana kwa furaha.
6Mjumbe Livingstone Lusinde kutoka Dodom
Post a Comment