Sunday, July 03, 2016

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni mbalimbali katika dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame, Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
 Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha mama Janeth Magufuli mara baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuondoka kwenye viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Post a Comment