Wednesday, July 20, 2016

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI


Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mbele) akitoka kukagua eneo lililoathirika na mmomonyoko wa ardhi eneo la Lukumburu Mkoani Njombe. 
Muonekano wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. 

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe alipotembelea kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotoa taarifa ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akisalimiana na Wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. 


Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimbeba mtoto aliyehudhuria kikao cha Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. 
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akicheza na wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe waliokuwa na furaha mara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. 
Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Iringa Bi. Elikael Manase akitoa maelezo kwa Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari ya mmomonyoko wa ardhi unavyoathiri sehemu ambayo Mkongo wa Taifa umepita eneo la Lukumburu Mkoani Njombe. 

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe. Wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

……………………………………………………………………………………………

Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 109.4 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Njombe ili kurahisisha huduma ya usafiri wa barabara kwa wakazi wa mikoa hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo mkoani Njombe wakati akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, kata ya Ulembwe, wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua barabara hiyo.Profesa Mbarawa amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo imetenga kiasi cha sh.bilioni 19 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

“Tumejipanga na tuna nia dhabiti kuhakikisha barabara hii tutaijenga kwa kiwango cha lami na katika kuharakisha kazi hii tutatafuta makandarasi wawili ili ujenzi huu ukamilike kwa haraka”, amesema Prof. Mbarawa.Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewataka wananchi kushirikiana na Makandarasi watakapoanza ujenzi huo ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kulete tija kwa wananchi wa Mikoa ya kanda ya kati.

Amesema kuwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Njombe upo katika hatua za kutangaza zabuni ili kupata Makandarasi wenye uwezo wa kujenga barabara hiyo kwa kuzingatia viwango kulingana na mkataba.Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Eng. Yusuph Mazana amesema kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makaete yenye urefu wa KM 109.4 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umekamilika na Mhandisi mshauri M/s Crown Teach Consult Ltd ameshawasilisha taarifa ya usanifu wa kina.

“Tumepokea taarifa ya usanifu wa kina kutoka kwa Mhandisi Mshauri hivyo tunahaidi kusimamia utekelezaji wa mradi huu kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani”,amesisitiza Eng. Mazana.Waziri Prof. Mbarawa ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo Mkoani Njombe.

No comments: