Friday, July 01, 2016

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIONEA URUSHAJI VIPINDI VYA BUNGE


Mhandisi wa mitambo wa Studio za Bunge Bi. Upendo Mbele akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake juu ya namna wanavyotekeleza majukumu ya kurusha vipindi kwa kuzingatia sheria na Kanuni za Bunge wakati wa Ziara iliyolenga kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kushoto) akifuatilia Kikao cha Bunge mapema Jana wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja .

Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti Bi. Justina Shauri akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake (hawapo pichani) wakati wa ziara yao Bungeni Mjini Dodoma ambapo walitembela Maktaba hiyo ili kujionea huduma zinazotolewa. 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof. Amon Chaligha akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma. Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Bunge Bw. Didas Wambura (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) na Ujumbe wake wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.(Picha na Frank Mvungi-Dodoma)
Post a Comment