Thursday, July 14, 2016

MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA ( TANTRADE) YATOA TUZO KWA MAKAMPUNI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka Akimkabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group Imani Kajula,.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) leo imeipa tuzo Kampuni ya EAG Group LTD kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kutangaza na kuhamasisha umma juu ya Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyoisha wiki iliyopita. 
 
Akikabidhi tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema ‘’ Leo la TanTrade ni kuchochea upatikanaji wa masoko ya uhakika na ukuzaji wa viwanda ili kuifanya Tanzania iwe fursa nyingi ya kukuza pato la Nchi na pia kutoa fursa kwa wafanya biashara wa Tanzania kukuza biasahara zao na maisha yao kwa ujumla.

Kwa upande wa EAG Group, Imani Kajula alisema ‘’ Hii ni farahi kubwa kwetu kuwa sehemu ya utafutaji ufumbuzi na kuchochea ukuaji wa biashara na hususani bidhaa za ndani kupitia utaalamu wetu wa masoko na biashara. Huu ni mwanzo mzuri unaotupa nguvu ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuchochea maendeleo ya Tanzania.
Post a Comment