Friday, July 29, 2016

PROPERTY INTERNATIONAL WADHAMINI TAMASHA LA UZINDUZI WA KITABU CHA SAFARI YA SOKA NCHINI, WATANI WA JADI YANGA, SIMBA, MABALOZI KUUMANA


 Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Machinga’, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
 Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kulia) amkimkabidhi Tisheti Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, zitakazotumika kufanyia mazoezi siku ya Tamasha. (wa pili kushoto) Katikati ni Afisa Habari wa Property, Saleh na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada.
 Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed, akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba, kuhusu Tamasha la jumamosi katika Uwanja wa Uhuru.
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
KAMPUNI ya Property International Ltd imedhamini bonanza la
uzinduzi wa kitabu cha soka cha Safari ya Soka la Tanzania litakalofanyika
Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika bonanza hilo la uzinduzi wa kitabu hicho litaambatana
na maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya uhuru wa Algeria, ambalo litahudhuriwa na Waziri wa
Habari Michezo na Utamaduni, Nape Nauye ambaye ataongozana na Waziri wa Mambo
ya Ndani Mwigulu Nchemba.
Katika Bonanza hilo pia kutakuwa na mechi kadhaa ikiwemo maveterani wa
timu za Simba na Yanga, mechi za vyombo vya habari pamoja na mabalozi wa nchi
mbalimbali nchini Tanzania wataungana na kucheza na maveterani wa Simba na
Yanga. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Post a Comment