Friday, July 22, 2016

MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE: MAFISI YALINGOJA MKONO UDONDOKE LAKINI YALIAMBULIA PATUPU

1
Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akiimba wimbo maalum kabla ya kufungua  Mkutano wa Halmashauri  Kuu ya CCM Taifa  (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.  Mkutano huo ni kwa ajili ya kupitisha jina la Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa CCM ambapo kesho atathibitishwa na Mkutano Mkuu Maalum kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma
Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe hao wakati akifungua mkutano huo amesema kikao hicho kilikuwa ni cha mwisho kwake kama mwenyekiti wa CCM , Akawashukuru wajumbe hao kwa kumpa ushirikiano kwa miaka kumi yote akiwa Mwenyekiti na akaongeza kwamba kama Chama cha Mapinduzi hakikupasuka mwaka jana hakiwezi kupasuka tena kitaendelea kudumu na kudumu zaidi.
Amesema Kulikuwa na mafisi yaliyokuwa yakingojea mkono udondoke tu ili yaweze kudaka na kula lakini yaliambulia patupu chama kilisimama kidete na kuendelea na mipango mizuri kwa ajili ya watanzania.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajab Luhwavi wakishiriki kuimba wimbo maalum wa CCM kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
3Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akfungua  Mkutano wa Halmashauri  Kuu ya CCM Taifa  (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
4Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua  Mkutano wa Halmashauri  Kuu ya CCM Taifa  (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. kutoka  kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
5Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua  Mkutano wa Halmashauri  Kuu ya CCM Taifa  (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
6
Msemaji wa CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Mzee Mark Mwandosya  katikati ni Mjumbe wa NEC kutoka mkoa wa Singida Ndugu Mwigulu Nchemba.
7
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC kutoka Zanzibar Ndugu Mohamed Abood akisalimiana na Mjumbe mwenzake kutoka Zanzibar pia Balozi Ali Karume katikati anayecheka ni Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Wilson Mukama.
8
Baadhi ya Wajembe wa NEC wakiwa kwenye mkutano huo kutoka kulia ni Mark Mwandosya, Profesa Peter Msola na Mzee Steven Wassira.
9
Mpiga picha wa Makamu wa Rais Bw. Adam Mzee kulia akiwaelekeza jambo waandishi wenzake kabla ya kuanza kwa mkutano huo kutoka kushoto ni  Emilian Malya kutoka Clouds Digital, Bakari Kimwanga kutoka Mtanzania na Said Mwishehe kutoka Jambo leo.
10
Mjumbe wa NEC Godfrey Zambi akisalimiana na Mjumbe mwenzake Hussein Mwinyi katikati ni Khadija Aboud.
11
Christopher Olesendeka akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake.
12
Baadhi ya wajumbe wakiwa tayari kwa mkutano huo
13
Wajumbe kutoka mkoa wa Pwani
14
Mzee Mark Mwandosya akizungumza na mjumbe mwenzake Peter Serukamba kutoka mkoani Kigoma
15
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa katikati akiwa na mkurugenzi wa Redio Uhuru Angela Akilimali kulia na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uhuru Selina Wilson wakiwa katika mkutano huo.
16
Wajumbe kutoka mkoani Mara wakiwa katika mkutano huo
17
Mwenyekiti wa CCM kotoka Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Kasheku Msukuma katikati akiwasikiliza wajumbe wenzake Januari Makamba kulia na Said Mtanda wakati  walipokuwa wakijadiliana jambo.
18
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa.
20Wajumbe wa NEC kutoka mkoani Kilimanjaro.
Post a Comment