Thursday, July 14, 2016

TRA YATOA MASHINE ZA EFD KWA WIZARA ZINAZOKUSANYA MADUHULI YA SERIKALI


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akimkabadhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya mashine tano kwaajili ya wizara yake ili kila wanapofanya malipo mbalimbali mapato ya TRA yakatwe.
 Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akionyesha
Mashine za Kiletroniki za EFDs ya mfano kabla ya kugawa kwa mashine tano
katika wizara zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
jijini Dar es Salaam leo, ambazo zitakuwa kwaajili ya kukusanya mapato
katika wizara hizo.
 Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akitoa maelekezo ya Mashine za Kieletroniki mbele ya makatibu wa kuu wa wizara pamoja na wawakilishi wa wizara mablimbali jijini Dar es Salaam leo kabla ya Kuanza kugawa katika wizara zote za serikali.


Baadhi ya Makatibu wa kuu wa wizara wakikabidhiwa mashine za Kieletroniki za
EFDs na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo
Kidata jijini Dar es Salaam leo.



Baadhi ya wawakilishi wa wizara mbalimbali za serikali wakiwa katika mkutano
wa kukabidhiwa mashine za Kieletroniki za EFDs jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
……………………………………………………………………………………
MAMLAKA
ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za Kieletroniki za EFDs tano
kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya
serikali kwa kutumia mashine hizo.

 Hatua
hiyo imetokana na agizo la  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na
mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa.

 Akizungumza
na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA,
Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za
serikali zitasaidia kutunza  kumbukumbu katika kupanga maduhuli.

“Mashine
hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha wananchi wanaopata huduma
wanapata risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa huduma
wanazopata”amesema Kidata.

Aidha amesema mashine hizo ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa.

Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia.

No comments: