Thursday, July 14, 2016

SUALA LA USALAMA KATIKA VIWANJA VYA NDEGE LINAHITAJI KUPEWA KIPAUMBELE

indexNa Masanja Mabula –Pemba
 MKUFUNZI kiongozi kutoka mamlaka ya viwanja vya ndege  Vedastus Ishengoma amesema kuwa suala la usalama katika viwanja vya ndege linahitaji kupewa kipaombele  cha pekee kwani bila ya kuwepo na usalama  hata mashirika ya ndege hayatafanya safari kwa hofu ya usalama wa maisha yao na mali zao.
Ishengoma aliyasema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanywa na mwandishi wa habari hizi , nje ya ukumbi wa mikutano wa kiwanja cha ndege cha Karume  nje kidogo ya  mji wa Chake Chake  katika mafunzo ya usalama kwa wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar  .
Alisema kwamba hakuna shirika la ndege ambalo linaweza kufanya safari zake sehemu ambayo haina uhakika na  usalama  wa abiria wake   .
Alisema kwamba mafunzo hayo yameandaliwa kimataifa ,kutokana na sheria za mashirika la ndege zinafanana  na usafirishaji wa anga hauna tofauti na hauna mipaka na ubaguzi .
“Mafunzo haya yameandaliwa limataifa , kwani sheria za mashirika ya ndege yahana tofauti ,mipaka wala ubaguzi kwa abiria , hivyo suala la usalama katika viwanja vya ndege linapaswa kupewa kipaombele ”alifahamisha .
Akizungumzia suala la viongozi kutokaguliwa wanaosafiri , alisema kwamb a suala hilo linaweza kuathiri wasafiri , kwani wakiona mmoja hakaguliwi na baadhi wanakaguliwa kunaweza kusababisha mashirika ya ndege kusitisha safari zake .
Mmoja  wa washiriki wa mafunzo hayo amesema  wao ni kuhakikisha kwamba kila abiria anapaswa kugakuliwa na atakeye kataa hataruhisiwa kusafiri na badala wataripoti katika vyombo vya sheria  na kuzungumzia suala la rushwa na kusema yanawezekana kutokea lakini kwa Zanzibar ni vigumu kutokea.
“Kama kuna kiongozi anakataa kikagauliwa , hatuwezi kumruhusu kusafiri na itabidi kuwasliana na vyombo vya ulinzi kwa hatua za kisheria ”alisisitiza Wacheni Maulid Vuai.
Kaimu Meneja wa mamlaka ya viwanja vya ndege Pemba Fatma Mohamamed amesema kwamba wamekuwa wakitoa elimu kwa viongozi juu ya kutambua usalama wakati wa kuingia .
Alifahamisha kwamba kutokana na elimu wanayoitoa viongozi wameanza kupata mwamko pamoja na uwelewa juu ya usalama , ambapo baadhi wameanza kutoa ushirikiano katika kufanikisha kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege.
Post a Comment