Wednesday, July 27, 2016

NHC ARUSHA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MRADI WA SAFARI CITY

indexNa Mahmoud -Ahmad Arusha
Shirika la nyumba la Taifa limeanza ujenzi wa nyumba za mfano kwa ajili ya uwekezaji wa
pamoja na wananchi katika kata ya Olmort jijini hapa mradi utakaojulikana kama
Safari city huku likikaribisha wananchi kuja kuwekeza kwenye mradi huo.
Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa shirika hilo mkoani hapa James Kisarika alisema
kuwa mji huo unajengwa kwa awamu na utakuwa na vitu vyote jamii inavyohitaji
ikiwemo maji, umeme na mtambo wa kuchakata maji taka.
Alisema kuwa kila kiwanja kitakuwa na huduma za bomba la maji,utengenezaji wa
barabara,uandaji wa hati miliki pamoja na michoro huku katika awamu ya kwanza
shirika likitoa haki za uendelezaji wa viwanja vyenye ukubwa wa mita za mraba
200-600 na yatapatikana kwa shilingi 35,000 tu kwa mita moja ya mraba.
“Mji huu ni miongoni mwa miji ya kisasa hapa nchini na utaweza kusaidia watu wa kada mbali
mbali kupata kumiliki nyumba na kujenga sisi tutakuwa wasimamizi wa mradi huu”alisema
kisarika
Alisema kuwa ili kuwa mmoja wa wawekezaji katika mradi huo unapaswa kufuata utaratibu kwa
kuchukuwa fomu ambayo ni bure na inatolewa na shirika hilo popote hapa nchini au
tembelea tovuti yao www.thesafaricity.comna utalipia asilimia 25% ya thamani ya kiwanja unachotarajia kununua.
 Aidha shirika la nyumba la taifa kupitia mradi huo linatoa fursa kwa makundi mbali
mbali ya wawekezaji wenye mahitaji ya uendelezaji wa nyumba za makazi kwa
vipato tofauti(chini,kati,na juu) majengo ya ofisi na biashara,maduka makubwa(Shoping
mall)pamoja na madogo,maeneo ya biashara,maendeleo ya viwanda vidogo
vidogo,burudani na utalii,Hospital.uwanda wa elimu,sanjari na huduma zote za
kijamii.
Baada ya  hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi
wa nyumba za mfano za mradi huo ikiwemo nyumba za makazi nafuu ambazo zitakuwa
za mfano kwa nyumba za makazi ambazo wawekezaji hao watatakiwa kujenga kwa
mfano huo.
Kutakuwepo na eneo la msitu pamoja na mashine maalumu ya kuchakata maji taka ambayo baada
ya kuyachakata maji hayo yatatumika tena kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mradi
huo.
Post a Comment