Friday, July 22, 2016

BENKI YA KIISLAMU YA AMANA YAZINDUA KITUO CHAKE KIPYA CHA HUDUMA KWA WATEJA


Meneja wa kituo cha huduma kwa Wateja Bw.Juma Msabaha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kilichozinduliwa hii leo Makao makuu ya Benki hiyo,Golden Jubilee towers Daresalam. Sasa wateja na wasiokuwa wateja wa benki hiyo wataweza kupata maelezo kuhusiana na mikataba ya mikopo inayofuata mifumo ya kiislamu, kutoa msaada katika matumizi ya huduma zetu mbadala kama ATM, Internet Banking, Amana Bank Mtaani, Amana Mobile na huduma nyingine mbalimbali. 
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakisikiliza kwa makini uzinduzi wa kituo hicho. Imeelezwa kuwa kituo hicho kitasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kutatua baadhi ya kero ambazo wateja walikuwa wanakutana nazo. 
Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI Bw. Munir Rajab akifafanua jambo kuhusu kituo hicho.


NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAM

BENKI ya Kiislamu ya Amana imezindua kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuboresha huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
 
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo hicho umelenga kuboresha mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Akifafanua kuhusu kituo hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa masaa 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa Amana na ambao bado hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.

“Tumejipanga vizuri, tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki ,watafafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia masuala ya akaunti,miamala ya kimtandao na huduma zinazotolewa na mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.

Ameongeza kusema Kituo hicho kitafanya kazi siku saba katika wiki,pamoja na siku za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo mbalimbali yanayowahusu wateja.

“Namba yetu ya huduma kwa mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni matarajio yetu kuwa wateja watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani ni rafiki kwa kila mmoja, imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi pamoja na njia zingine za mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha

No comments: