Saturday, July 30, 2016

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) na baadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitazama  jeneza lenye mwili wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeneza hilo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. Marehemu Senga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Mwili wa marehemu utalala nyumbani kwake Sinza na Jumapili Julai 31, ibada ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika kwenye viwanja vya Sinza uzuri na baadaye safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Kwimba alikozaliwa itaanza na mazishi yatafanyika huko. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

 Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili
 Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
 Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea.


Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili
Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka

No comments: