Thursday, July 28, 2016

“TUNAWEZA KUBADILISHA MAISHA YA WAAFRIKA KAMA TUKIACHA BIASHARA ZA MAGENDO”- THABO MBEKI

Benjamin Mkapa
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wa Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Sipho Nkosi
Rais wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa Madini nchini Afrika Kusini, Sipho Nkosi akitoa hotuba kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Sipho Nkosi at African Leadership Forum 2016 Tanzania
Thabo Mbeki
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mh. Thabo Mbeki akichangia mada katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
High table at the African Leadership Forum 2016
Kutoka kushoto ni Rais wa zamani wa Namibia, Mh. Hifikepunye Pohamba, Rais wa zamani wa Mozambique, Joaquim Chissano, Rais mstaafu, Mh. Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mh. Thabo Mbeki pamoja na Rais wa zamani wa Mozambique, Mh. Armando Guebuza wakiwa meza kuu katikaKongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mwakilishi wa vijana kutoka Nigeria
Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Nigeria akishiriki kwenyeKongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mfanyabiashara na mmliki wa makampuni ya Excel Management, Mikono Speakers na Focus Outdoor Deogratius Kilawe
Mfanyabiashara na mmliki wa makampuni ya Excel Management, Mikono Speakers na Focus Outdoor Deogratius Kilawe akitoa maoni katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Tanzania former Prime Minister
Mawaziri wakuu wastaafu kutoka kushoto ni Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. John Malecela pamoja na Mh. Cleopa Msuya walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
_MG_0415
Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lilioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na kuratibiwa na Uongozi Institute.
_MG_0422
_MG_0429
_MG_0432
_MG_0458
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amezungumzia biashara ya magendo ya madini ya Tanzanite katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) kuzungumzia namna ya kuzifanya biashara kuleta mabadiliko chanya barani Afrika.
Mbeki ameyasema hayo katika kongamano hilo lililowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika kujadili jinsi biashara inavyoweza kusaidia kubadili maisha ya Waafrika lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro, Dar es salaam.
Aidha, Mbeki amesema takribani dola milioni 800 hupatikana kila mwaka kwa kuuza na kusafirisha madini ya Tanzanite nchi za nje, lakini kutokana na biashara za magendo na wizi wa madini ya Tanzanite ni dola milioni mia tano tu hupatikana kila mwaka nchini Tanzania
Ameongeza kuwa Tanzania inasafirisha kiwango kidogo cha madini hayo ukilinganisha na uchimbaji halisi unaoendelea kila mwaka, na hivyo kufanya sekta ya madini pamoja na biashara kuzorota kwa hali ya juu
Tanzania ni nchi pekee duniani inayochimba madini ya Tanzanite yenye thamani kubwa lakini nchi za Afrika Kusini na Kenya ndiyo zimekuwa zikijulikana kwa uuzaji wa madini hayo.

Mkutano huo unataraji kufanyika kwa siku mbili na kudhaminiwa na mashirikia na taasisi mbalimbali ikiwepo Taasisi ya Mo Dewji (Modewji Foundation.
Post a Comment