Thursday, July 14, 2016

WAZIRI MWAKYEMBE, MASAUNI WAFANYA ZIARA MKOANI GEITA, WAZUNGUMZA NA UONGOZI GGM, WATEMBELEA GEREZA CHATO


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya mkoani Geita (GGM) pamoja na Viongozi wa Serikali wa mkoa huo, kuhusiana na masuala mbalimbali ya utatuaji wa migogoro iliyopo kati ya GGM na wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo. Waziri Mwakyembe aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, katika ziara hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati), na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi zilizofanywa na viongozi hao wa Wizara. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM), Terry MulPeter akizungumza katika kikao kati ya uongozi wa kampuni yake na viongozi wa serikali uliokuwa unaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hawapo pichani). Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo katika kikao cha viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM) cha kujadiliana masuala mbalimbali ya utatuzi wa migogoro kati ya kampuni hiyo na wananchi wanaoishi jirani na kampuni hiyo. Kikao hicho ambacho kiliongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wanne kulia) ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga. Wa pili kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto kwa Dk Mwakyembe), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati ya Dk Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa) pamoja na viongozi wengine wakitoka kulikagua Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo ndani ya Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani Geita. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Edward Kaluvya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (aliyevaa kaunda suti) akichomolewa ndani ya gari lake lililopinduka katika Kijiji cha Bwanga wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wakati dereva wa gari hilo alipokuwa anamkwepa mwanafunzi aliyekatisha ghafla barabarani wakati wa msafara wa ziara ya kikazi wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (kulia aliyevaa kofia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari mjini Chato, mkoani Geita mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto). Katika ziara yao licha ya kufanya majukumu mengi ila walifanikiwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini mkoani Geita (GGM) na pia walilikagua Gereza Chato linalojengwa mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment