Tuesday, July 05, 2016

TRA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA ZA MAGENDO

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) itaendelea kudhibiti na kupambana na biashara za magendo katika vituo mbalimbali ambavyo vinaendelea na vitendo vya magendo.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 

Amesema TRA itazidi kupambana na kuziba mianya yote ya  upotevu wa mapato hususani katika msisitizo wa matumizi wa Mashine za Kieletroniki za kodi za EFDs pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara na kufuatilia madeni.

Pia amesema kuwa TRA itaendelea kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine za Kieletroniki za kodi za (EFDs) kwa kuwakamata na kuwatoza faini au kuwafikisha mahakamani na kuwachukulia hatua za kisheria ili kuhakikisha inafikia na kuvuka malengo.

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeshagawa mashine za Kieletroniki za EFDs 1120 kwa wafanyabiashara wanaostahili kupata mashine hizo bure na ambao hawajachukua machine za kieletroniki za kodi za EFDs ili kuwezesha TRA kukusanya mapato ya Serikali.
Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akifafanua juu ya Operesheni ambayo itatumika katika makusanyo ya ndani ambapo watapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa na fremu kwa fremu katika kugawa Mashine za Kieletroniki za EFDs kwaajili ya Kukusanya kodi kwa kila Mfanyabiashara Kushoto ni  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuvuka lengo la makusanyo ya Kosi kwa mwaka 2015/2016.Kulia ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya.
Kushoto ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya  viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mtafiti Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Beldo Chaula akifafanua juu ya makato yanayokatwa kwenye taasisi za fedha hapa nchini kuwa zitatozwa kwa taasisi hizo za fedha kwenye Miamala na sio kwa kila mwananchi.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Post a Comment