Thursday, September 03, 2015

SERIKALI YAAHIDI KUZIDI KUPIGA JEKI WAFANYAKAZI WA AFYA YA JAMII KUBORESHA AFYA YA JAMII VIJIJINI


Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, Profesa Japhet Killewo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. 
Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
Mkurugenzi Msaidizi, Ukuzaji Afya Bi Hellen Semu, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXx

 Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI ya Tanzania imeelezea utayari wake wa kupiga jeki na kuwajumuisha wafanyakazi wa afya ya jamii katika nguvukazi ya sekta ya afya (national health workforce) ya taifa ili kuboresha afya ya jamii hususani katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii (Community Health Worker Learning Agenda Project - CHW-LAW) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo alisema ni muhimu kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya ya jamii ili kukidhi mahitaji ya kijamii. 

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Dkt Neema Rusibamayila, Msemo aliwaasa wadau kufanya tafiti ya kisayansi ili kukabiliana na hali ya upungufu wa wafanyakazi wa afya ya jamii, ambao umekuwa ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma za kiafya nchini. 

Msemo alipongeza hatua ya wadau hao kwa kuzungumzia masuala ya wafanyakazi wa afya ya jamii pamoja na kuja na mradi utakaowezesha wafanyakazi hao kupata mafunzo ya kila mara ili kuboresha utendaji wao katika utoaji wa huduma ya afya ya jamii. 

Alisema wafanyakazi wa afya ya jamii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa pia katika uboreshaji wa sekta ya afya haswa katika magonjwa ya malaria, kifua kikuu, VVU/Ukimwi, afya ya Uzazi na mtoto. 

Naye, Profesa Japhet Killewo, ambaye ni Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, alisema lengo la semina hiyo ya siku nzima iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam lilikuwa ni kuwakutanisha pamoja wadau katika afya ya jamii pamoja na wahisani kujadili utekelezaji wa utafiti uliofanywa na njia bora za kuiboresha na kuikuza sekta ya afya nchini. 

Killewo alisema kuwa wafanyakazi wa afya ya jamii wamekuwa kwa miaka mingi wakikosa kutambuliwa kwa kuwa wengi wao walikuwa darasa la saba na wahitimu wa kidato cha nne, wengi wao mbali ya kuwa na uzoefu, wamekuwa wakifanya kazi za kuijtolea bila mshahara. 

Alisema kuwa hilo limechangia kukosekana kwa jitihada madhubuti ya kazi miongoni mwao. 

Alisema kuwa na ndiyo sababu CHW-LAW, wakishirikiana na serikali na wahisani ambao ni pamoja na USAID, Muhas na Johns Hopkins wameamua kuandaa semina hiyo kwa wafanyakazi wa afya ya jamii. 

Alisema kuwa semina hiyo, ambayo pia itafanyika mwezi oktoba, itafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Kigoma, Simiyu, Shinyanga na Tarime, ambayo ipo katika mpango wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now). Ambapo wapatao wafanyakazi 300 wa afya ya jamii wanatarajia kuudhuria. 

Alisema semina kama hizo zikipewa msukumo na serikali na wahisani mbali mbali pia zitafanyika katika mikoa mingine nchini. 

No comments: