Wednesday, July 08, 2026

MBUNGE WA BUNGE LA NORWAY AVUTIWA NA VIVUTIO VYA SERENGETI, AIKARIBISHA DUNIA KUTEMBELEA TANZANIA


Mbunge wa Bunge la Norway, Mhe. Himanshu Gulati, akiongozana na mwenyeji wake, Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ametembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na kujionea vivutio vya kipekee vya utalii, wanyamapori mbalimbali pamoja na mandhari ya kuvutia inayoifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa utalii duniani.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mhe. Gulati alisema amefurahishwa na ubora wa vivutio vya utalii nchini pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhifadhi rasilimali za asili na wanyamapori kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, amewahamasisha wananchi wa Norway na mataifa mengine duniani kuitembelea Tanzania ili kujionea uzuri wa Hifadhi za Taifa, urithi wa asili na uzoefu wa kipekee unaopatikana katika vivutio vya utalii vya nchi hii.

"Tanzania ni nchi yenye vivutio vya kipekee na mazingira ya kuvutia. Kila mtu anapaswa kupata nafasi ya kuitembelea na kujionea uzuri wake," alisema Mhe. Gulati.

No comments:

MBUNGE WA BUNGE LA NORWAY AVUTIWA NA VIVUTIO VYA SERENGETI, AIKARIBISHA DUNIA KUTEMBELEA TANZANIA

Mbunge wa Bunge la Norway, Mhe. Himanshu Gulati , akiongozana na mwenyeji wake, Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo , ametembelea...