Saturday, September 05, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AMNADI MGOMBEA UBUNGE NDUGU HASSAN KAUNJE NA MADIWANI LINDI MJINI

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Msinjahili katika Manispaa ya Lindi kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October, 2015. Kushoto kwa Mama Salma ni mgombea wa ubunge katika jimbo hilo Ndugu Hassan Kaunje.
4Mke wa Rais na MNEC Taifa anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na wananchi wa Lindi Mjini (hawapo pichani) wakati akimnadi Ndugu Hassan Kaunje anayegombea ubunge katika jimbo hilo pamoja na madiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi tarehe 4.9.2015.
2
Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye kampeni za kumnadi Mgombea ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini wakishuhudia hotuba mbalimbali  zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Kata ya Msinjahili tarehe 4.9.2015.
3
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwa ameshika bango la mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akimnadi kwa wananchi wa Lindi Mjini.  Aliyeshika bango hilo  kushoto ni Mgombea ubunge katika Jimbo la Lindi Mjini Ndugu Hassan Kaunje na katikati ni mgombea udiwani wa kata ya Msinjahili Mama Asina Kawamba.
PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: