Saturday, September 12, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:NATAKA TANZANIA IWE NCHI YA VIWANDA

1

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Meatu mkoani Simiyu wakati alipofanya mikutano mbalimbali katika wilaya za Busega, Meatu, Bariadi na Itilima akiwaomba wananchi wa wilaya hizo kumpigia kura za ndiyo ili kuwa rais wa Tanzania na kuwatumikia watanzania katika nafasi hiyo kubwa.
Amewaambia wananchi hao kwamba ametekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini kwa mafanikio akiwa Waziri wa Ujenzi na alikuwa akitumwa,  Lakini sasa atakuwa akiwatuma yeye watendaji na kuwasimamia. Jukumu ambalo yeye binafsi anaweza kulitekeleza kwa mafanikio makubwa, uaminifu, uchapakazi na ukweli ili kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa watanzania wa kipato cha chini lakini pia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ameongeza kwamba anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana waliowengi na kukuza uchumi wa taifa kuptia sekta hiyo ya viwanda ambapo ameelezea kwamba serikali yake itajenga viwanda Vodogo, Vya kati na Vikubwa ambayo vinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali kama mikoba, mikanda, viatu, Nguo na bidhaa nyingine nyingi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SIMIYU)
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wake wa kampeni mjini Meatu mkoani Simiyu leo.
34
Umati wa wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo uliofanyika mjini Meatu mkoani  Simiyu.
5
Baadhi ya Vijana wa Meatu wakiwa juu ya mti na bendera zao wakipata ujumbe wa Dr John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
6
Akina mama wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Dr, John Pombe Magufuli.
7
Wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akimwaga sera zake.
8
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano mjini Meatu.
9
Msanii Emmanuel Mbasha akiwa katika mkutano huo.
10
Wasanii wa ngoma za kisukuma wakiwa wamevakia mithiri ya ndege aina ya Tai wakiwa katika mkutano huo ili kutoa burudani.
12
Kijana huyu akiwa amevaa kofia yake aina ya Pama huku ikiwa imevalishwa vipeperushi vinavyosema Magufuli “Hapa ni  Kazi Tu”
13
Mgombea ubunge wa jimbo la Itilima Ndugu Silanga Njalu akiwaomba kura wananchi wa Nanga wilayani Itilima.
14
Mama huyu akionyesha mapenzi yake kwa mgombeaubunge wa jimbo la Itilima Ndugu Njalu Silanga.
15
Ngoma zimepigwa sasa ni wakati wa kusikiliza sera za Dr. John Pombe Magufuli.
22
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Busega  Paul Mzindakaya huku Dr. Titus Kamani Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu akisikiliza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Lamadi.
21
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Lamadi mkoani Simiyu.
20
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoawa Simiyu Dr. Titus Kamani wakati alipokuwa akimnadi katika kijiji cha Mkula.
19
Hapa ni Magufuli tuuu!!
18
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwasili katika mji wa Bariadi kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
23
Mgombea ubunge wa jimbo la Busega  Dk Chegeni akiomba kura mjini Lamadi Busega.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwapigia debe wagombea ubunge na udiwani Meatu.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Msanii Mr Blue akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Meatu leo.
????????????????????????????????????
Vijana wa Orijino Komedi wakitumbuza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akifurahia onesha la vijana wa orijino Komedi.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Shishi Baby Shilole akifanya vitu vyake jukwaani mjini Meatu wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini humo.
????????????????????????????????????
33
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la mkutano mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika mjini Meatu mkoani Simiyu leo.

No comments: