Saturday, September 12, 2015

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YAANDAA MRADI WA KUBORESHA MAENEO MATANO YA WAZI YA MJI WA ZANZIBAR


md1
Mkuu wa Ushirikiano wa  Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na  Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
md2
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua  Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma.
md3
Msaidizi  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya Landscape ya Switzerland Roland Raderschall akitoa maelezo ya  Mradi wa  mwanzo wa kuboresha  Kiwanja cha Demokrasia cha Kibandamaiti katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
md4
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Zanzibar Muhamad Juma akitoa ufafanuzi kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha eneo la wazi  la Kibandamaiti., (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
md5
Ramani ya maeneo matano ya wazi yatakayofanyiwa uboreshaji na Idara ya Mipango na Vijiji ambayo ni Kibandamaiti, Lumumba, Darajani, Chumbuni na Darajabovu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Post a Comment