Tuesday, August 18, 2026

RAIS TSHISEKEDI AFANYA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA

 Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ampokea Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Ndogo ya Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Ikulu Ndogo ya Zanzibar, tarehe 18 Agosti, 2026



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, katika Ikulu Ndogo ya Zanzibar, akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya mazungumzo yatakayojikita katika kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na DRC, sambamba na kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja kwa mataifa hayo mawili.

Tanzania na DRC zina uhusiano wa muda mrefu wa kihistoria na kidugu, huku ushirikiano wao ukiendelea kuimarika katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa jitihada za kuimarisha diplomasia, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

RAIS TSHISEKEDI AFANYA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA

 Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ampokea Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Nd...