HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN! Taarifa zaidi zitawajia baadaye. SOURCE: GLOBALPUBLISHERS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WAZIRI MKUU: SERIKALI YAENDELEA KUHAKIKISHA MAFUTA HAYAADIMIKI NCHINI
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini unaendelea ...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
Pascal Mayalla akiwa katika chumba cha wagonjwa Daraja la kwanza katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako amelazwa kwa matibabu baada ya ku...


1 comment:
R.I.P Uncle J. Nyaisanga
Post a Comment