Thursday, March 03, 2016

RAIS MAGUFULI NA RAIS KENYATTA WAWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA YA ARUSHA-HOLILI/TAVETA-VOI

HOL1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Tengeru nje kidogo ya Jiji la Arusha mara baada ya kuwasili  kwa ajili ya Uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni  kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa kabla ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwaongoza Marais wa Kenya, Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini pamoja na Burundi kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia mti maji pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya sherehe za unzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
HOL10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi.
HOL11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali  Mohamed Shein mara baada ya sherehe za uzinduzi wa barabara hiyo kukamilika.
HOL12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara hiyo ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, wameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili – Taveta – Voi, yenye urefu wa kilometa 234.3 ambayo inaunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la Msingi imefanyika katika eneo la Tengeru Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Dkt. Joseph Butore, Mwakilishi wa Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki wa Rwanda Mheshimiwa Valentine Rwabiza na Makamu wa Pili wa Rais Sudan Kusini Mheshimiwa James Wan Iga.
Uzinduzi huo pia umehudhuria Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kwa upande wa Tanzania ujenzi wa barabara hiyo unatakelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Arusha hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1, na ujenzi wa barabara ya mzunguko yaani “Bypass” yenye urefu wa kilometa 42.4. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Tengeru hadi Usa River yenye urefu wa kilometa 8.2 na Kutoka Usa River hadi Holili mpakani mwa Kenya na Tanzania yenye urefu wa kilometa 100.2
Gharama za upanuzi wa barabara ya Arusha – Tengeru na barabara ya kuzunguka nje ya jiji la Arusha kwa upande wa Tanzania ni shilingi bilioni 209.6, ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) itatoa mkopo wa shilingi bilioni 190.2 na serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 19.4.
Aidha Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo kwenye mazungumzo na serikali ya Japan ili kupata mkopo wa ujenzi wa awamu ya pili inayoanzia Tengeru hadi Holili.
Kwa upande wa Kenya, mradi huu unahusisha ujenzi wa barabara mpya kwa sehemu ya Taveta hadi Mwatate yenye urefu wa kilometa 100. Sehemu ya Mwatate hadi Voi ujenzi wake umekamilika.
Akizungumza katika hafla hii, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema wananchi wa Afrika Mashari hawapaswi kuwa masikini na kueleza kuwa mradi huo na mingine itakayotekelezwa chini ya ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi.
Kwa upande wao Marais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na wawakilishi wa marais wa Burundi, Rwanda, Sudani Kusini wameuelezea mradi huo kuwa ni moja ya miradi muhimu ya kuimarisha uchumi wa jumuiya ya Afrika Mashariki na wametoa wito kwa nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo kushirikiana kukuza biashara baina yake.
Viongozi hao wote wamekiri kuwa Jumuiya hii yenye watu zaidi ya milioni 160, inayo nafasi ya kupiga hatua kubwa za kiuchumi na kuondokana na umasikini, ikiwa italitumia vizuri soko la pamoja kwa kubadilisha bidhaa kutoka nchi moja hadi nyingine na kujenga viwanda vingi badala ya kuendelea kutegemea bidhaa kutoka nje.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
03 Machi, 2016

No comments: