Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halmashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesisitiza fedha za Elimu ambazo zimetolewa na Serikali kama zawadi katika Halmashauri mbalimbali zilizofanya vizuri katika Sekta ya Elimu zitumike vizuri.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati wa kutoa zawadi kwa Halmashauri 10 ambazo zimepokea Shilingi Bilioni 15.5.
Halmashauri hizo ni Mbinga, Chato, Busega, Lushoto, Niyankasi, Liwale, Sikonge, Mbarali, Mpanda, pamoja naTabora.
Pia, Profesa Ndalichako amezitaja Halmashauri 10 za mwisho kuwa ni Rombo, Kiteto, Meatu, Mafinga, Kasulu, Butihama, Wanging’ombe, Mbozi na Makambako.
Kwa upande wake, WaziriwaNchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene amezitaka Halmashauri hizo ambazo zimefanya vizuri na kupata zawadi hiyo ya fedha kuzitumia vizuri fedha hizo na kuhakikisha Elimu Bora inapatikana.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akimkabidhi hundi bilioni 15,532,905.10 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa halmashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya akionesha cheti alichopewa kama halmashauri iliyoshika nafasi ya kwanza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali Bw. Yeremiah Tito Mahinya akipokea cheti pamoja na zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya halmashauri ya wilaya ya Mbarali kufanya vizuri katika suala la elimu. Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Bw, Ahmada .A. Suleman akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wilaya hiyo kufanya vizuri kielimu, wa pili kutoka kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa, George Simbachawane
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halimashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya akitoa neno la shkukrani kwa niaba ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla fupi ya utoaji zawadi kwa halmashauri zilizofanya vizuri.
Baadhi ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halimashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Picha ya Pamoja.
Kaimu Afisa elimu MsingiMoses Ndanzlama(kushoto), Afisa Elimu Sekondari Bi. Claudia Kita(katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali Bw. Yeremiah Tito Mahinya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupewa zawadi ya Cheti.
Comments