Tuesday, March 08, 2016

NAPE:TUTATENGENEZA SERA MADHUBUTI ILI SEKTA YA FILAMU IWE RASMI

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea  Tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili barani Afrika ambayo imetwaliwa na msanii Single Mtambalike a.k.a Richie (katikati, kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na wapili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA)  leo jijini Dar es Salaam.Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah ,Mwambene(kushoto) na kulia ni Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia waliokaa ni Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kishwahili barani Africa, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa Filamu walioiwakilisha nchi katika mashindano ya Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Msanii wa Kitanzania anayeishi Marekani Honey Moon.Hafla hiyo imeambatana na kukabidhiwa vyeti vyapongezi kutoka Serikalini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah ,Mwambene akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Ambapo wasanii hao walikabidhiwa Vyeti vya pongezi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kukuza tasnia hiyo hapa nchini.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kutwaa Tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili Barani Afrika msanii Single Mtambalike a.k.a Richie leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.Tuzo hiyo imetokana na mashindano ya Tuzo za Fiolamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) yanayofanyika nchini Nigeria ambapo wasanii sita kutoka Tanzania walishiriki na wawili kuibuka na ushindi ambapo mshindi mwingine ni Lulu Michael.aliyeshinda Tuzo ya Filamu Bora Afrika Mashariki.
Post a Comment