Monday, March 07, 2016

AIRTEL FURSA YAWEZESHA VIJANA KWA MILIONI 15 MANYARA.

Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo  kwa  Kijana Frank Rowland ( katikati)  kabla ya kumkabidhi banda la kuku la kisasa na kuku  100 wa kienyeji  kutoka Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA wa kuwezesha vijana hapa nchini  katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Wanaoshuhudia ni ndugu zake Frank na wafanyakazi wa Airtel waliojumuika katika hafla hiyo.
 Kijana Frank Rowland (wa pili kushoto) anayejishughulisha na ufugaji wa kuku , akitoa maelekezo  kwa Afisa uhusiano na matuki wa Airtel Dangio Kaniki ( wa pili kulia) na Meneja wa mauzo kanda ya Manyara Peter Kimaro (kushoto) jinsi anavyotunza kuku baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa  banda la kuku la kisasa na kuku  100 wa kienyeji , kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Akishuhudiwa na mama yake Doris Kombe (kulia)
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel , Dangio Kaniki (wa pili kulia) akipiga makofi pamoja na mama yake na Kijana aliyewezeshwa na Airtel Fursa   Doris Kombe (kushoto) na wafanyakazi wengine wa Airtel  wakati  wa hafla ya kumkabidhi vifaa hivyo Kijana Charles Samuel (wa pili kushoto).
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles Samuel (wa pili kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, kadi ya pikipiki kama baadhi ya misaada aliyopatiwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa, Babati mjini hapo jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore ( kulia), afisa mauzo kanda ya Babati Johnson Zephania (katikati) na mama yake mzazi Charles Doris Kombe (kushoto)
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles Samuel (kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na pikipiki kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa, Babati mjini hapo jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore ( kulia) na afisa mauzo kanda ya babati  Johnson Zephania  (wa pili kushoto).

·        Wajasiliamali kupatiwa vitendea kazi vya milioni 20 kila wiki na Airtel FURSA.
 KMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeendelea kutoa msaada kwa vijana mkaoni Manyara wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 wakiwa na lengo la kutimiza dhamira yake ya kuwawesha vijana nchini kuweza kujipatia kipato na ajira.

Akizungumza Mkoani Manyara Meneja Mauzo wa Airtel Brighton Majwala amesema “Airtel FURSA baada ya kuendesha semina ya Ujasiliamali mwezi uliopita tulikutana na zaidi ya vijana 300 walijitokeza nakuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira. Leo hiii tumekuja kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

Kwa upande wake Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki ameeleza kuwa “Airtel tuko tayari kutumia zaidi ya milioni 20 kila wiki kuwawezesha vijana wanaojitokeza na kuonyesha wanania ya kujiendeleza hapa nchini’.

Nae kwa upande wake  kijana Frank Rowland kutoka wilaya ya Hanang aliyewezeshwa na Airtel Fursa alishukuru kwa kuwezeshwa na Airtel, sitakaa bure, ntahakikisha ninauendeleza mradi huu unisaidie kimaisha na kuwawezesha pia vijana wenzangu kupata ajira ntakazo wapa" alisema Frank.

Kijana mwingine aliyenufaika na Airtel Fursa ni fundi umeme, Charles Samuel, mkazi wa mtaa wa Nakwa, Babati mjini, ambaye amepewa msaada wa pikipiki na vitendea kazi vingine kwaajili ya kufanyia biashara ya kutembelea wateja watakaohitaji huduma yake ya ufundi.

Charles aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa usafiri na zana alizozipata zitachochea mafanikio yake kimaisha na kuwataka vijana wenzake kuchangamkia fursa zinazotolewa na Airtel ili waweze kuondokana na umasikini

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Katesh, wilaya ya Hanang, Michael Severine, ameishukuru kampuni ya simu ya Aitel kwa kutimiza ndoto za vijana kiuchumi kupitia mradi huo wa Airtel Fursa.

"Tulikuwa tunaambiwa  watu wanatoa hongo ili wapatiwe mitaji kwa njia ya upendeleo, na Airtel lakini kwa kumwezesha kijana mjasiriamali wa Hanang, tena kwenye kitongoji cha Katesh 'B", nimebaini kuwa ni uongo na uzushi" aliongeza mwenyekiti huyo.

No comments: