Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la kinondoni haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda leo jijini Dar es Salaam.
Wakili mshitakiwa Juma Nassoro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. juu ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni .Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akitoka Mahakani hapo mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CUF) iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Idd Azzan imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kuu ya Tanzania.
Juma Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa Kinondoni amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo amemuaomba msajili kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya kupangiwa tarehe nyingine.
Kwa upande wa Mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda.
Comments