Wednesday, March 09, 2016

PROF. MBARAWA; TUMIENI DATA CENTRE KUTUNZA TAARIFA ZENU

AR1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfumo wa ufatiliaji wa kielektroniki katika jengo la kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi  rasmi mwezi Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda.
AR2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
AR3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi  rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
AR4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo hicho cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa (data centre) kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote.
Akizungumza baada ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya Mawasiliano amesema asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali.
Waziri Mbarawa amezitaka taasisi za Benki, Simu, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma za kituo hicho.
Amesema huduma ya mtandao katika kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na mkongo wa taifa na hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa kwa haraka.
Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinalimikiwa na Serikali.

No comments: