Friday, March 18, 2016

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara
Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina  Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina  Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo

Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa, Raymond Mndolwa  wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.

Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.



Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif.
Mradi wa Mwongozo unavyoonekana kwa juu 
Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.
Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.

No comments: